KASHFA: Taasisi kubwa ya taasisi ya fedha duniani ilivyosaidia ukwepaji mkubwa wa kodi!

Feb 9, 2015

 HSBC Bank in Switzerland

HSBC Bank (plc) moja ya taasisi kubwa kabisa za fedha duniani imeingia katika kashfa kubwa ya 'kusaidia' wafanyabiashara, wanasiasa na watu maarufu kukwepa ulipaji stahiki wa kodi na ufichaji wa mamilioni ya fedha katika benki mbalimbali duniani.
Taasisi ya HSBC ya nchini Uingereza ilisaidia pia wahalifu wa kimataifa, wauza silaha hasa wa wanaopatikana nchi za Afrika, ma-dikteta wavunja sheria wa namna mbalimbali kurahisisha 'shughuli'zao huku kodi kubwa ikikwepa katika njia ambazo hazikua sahihi.

 Ripoti iliyotolewa siku ya Jumapili baada ya uchunguzi yakinifu wa makabrasha ya siri  uliofanywa na maripota wapatao140 kutoka taasisi ya International Consortium of Investigative Journalists (ICIJ) ilionyesha kuwa, benki ya HSBC ilikua ikipata faida kubwa sana kutokana na 'uharamia' waliokua wanafanya.

Taarifa ya utetezi iliyotolewa na afisa wa HSBC inasema benki hiyo itawajibika kutokana na makosa hayo na kuongeza kuwa kampuni tanzu ya benki hiyo ya nchini Uswisi iliyosababisha upotevu huo mkubwa wa kodi haikufata taratibu stahiki katika utendaji wake wa kazi.
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team