Wananchi saba kati ya kumi (69%) wanasema rushwa zilizoripotiwa kwenye
ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
ni upotevu wa fedha zao (za umma). Zaidi ya nusu ya wananchi (55%)
wanaamini kuwa aina hii ya rushwa inagusa sana maisha ya yao ya kila
siku, na watatu kati ya kumi (31%) wangependa kutaarifiwa kuhusu matokeo
ya ukaguzi kupitia vipindi vya redio vinavyorushwa kila wiki kwa muda
wa nusu saa.
Wananchi pia wanaamini kuwa Rais
anapaswa kuchukua hatua juu ya matokeo ya ripoti ya CAG: Takriban wananchi sita kati ya kumi (57%) wanaamini kuwa Rais anawajibu wa kufuatilia masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali. Taasisi nyingine zinazotajwa kuwa na wajibu wa kufanya hivyo ni pamoja na Baraza la Mawaziri (16%) na mahakama (11%).
Mbali na Rais, hakuna taasisi au mtu binafsi aliyetajwa na wananchi kwa zaidi ya 20% kuwa anawajibu wa kushughulikia masuala ya ukaguzi wa hesabu za serikali.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari mfupi wenye jina la Walezi wa Uwajibikaji: Ufahamu na maoni ya wananchi kuhusu taasisi za usimamizi. Muhtasari huu umetokana na takwimu kutoka utafiti wa Sauti za Wananchi,
utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika
mara kwa mara kwa njia ya simu za mkononi. Matokeo yametokana na
takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,474 katika maeneo
mbalimbali Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya) kati ya
miezi ya Septemba na Oktoba 2014.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za wazi juu ya makosa ya rushwa na haja ya
Rais kuchukua hatua, wananchi wana hisia kinzani linapokuja suala la
adhabu kwa viongozi wenye matumizi mabaya ya fedha za umma. Mwananchi
mmoja tu kati ya ishirini (6%) anafikiri kuwa wale wanaopatikana na
hatia ya rushwa wanapaswa kuondolewa katika ofisi za umma, na ni mmoja
tu kati ya wananchi sita (15%) anayefikiri kuwa wala rushwa wanapaswa
kufungwa. Adhabu sahihi kwa wala rushwa iliyotajwa na wananchi wengi
(32%) ni kufukuzwa kazi, kunyang’anywa pensheni, kunyang’anywa mafao na
kulipa pesa walizofuja (30%).
Chanzo: Twaweza.org