| Askari magereza wa Shimo La Tewa Maximum Security Prison akiwa amekaa sambamba na wafungwa kutoka gereza hilo wakisubiria matibabu katika hospitali ya Coast General Hospital siku ya jana tarehe 20 Mei, 2015 kutokana na mlipuko wa Kipindupindu. |
Kenya;
Wafungwa waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo wa mlipuko wametajwa kuwa ni Hamisi Guzo Samba, Eric Omondi Odhiambo aliyekuwa ameshtakiwa kwa kosa la wizi na mtu wa tatu jina lake halikuweza kupatikana wakati habari hii inaandaliwa.
Shimo La Tewa Maximum Security Prison, gereza walilokuwamo wafungwa hao limekumbana na adha hiyo baada ya mmoja wa wafungwa aliyeingia siku chache kabla ya mlipuko kuhisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu.
Coast Region Prison Commander James Kodieny amesema wafungwa wengine waliothirika na Kipindupindu tayari wametengwa (karantini) ili kuzuia ulipuko usisambae zaidi. Mpaka sasa idadi ya watu 79 wamesharipotiwa taarifa zao katika hospitali ya Coast General Hospital. Wafungwa waliobakia gerezani wamepewa dawa aina ya prophylaxis ambayo ni 'antibiotiki' ili kuwakinga na maambukizi zaidi, taarifa ya Dr Mary Ochola imesema.