Kwa lugha ya kiingereza tunasema ''These are the brains behind this great invention''..... Time Tickets!
Time Tickets ni App iliyotengenezwa na vijana wabunifu wenye asili ya Tanzania walioona 'gap' kubwa kati ya utumiaji sahihi wa simu za mkononi kupitia huduma za mobile money services na ununuaji wa tiketi kwa ajili ya matamasha mbalimbali yanayofanyika nchini kote. Kutana na Goodluck Akyoo, Josephat Mandara na Mwasapi Kihongosi.
Neno TIME ni kifupi cha maneno haya: Tickets Made Easy
Katika bara linalorekodi idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi huku huduma za kifedha kupitia simu ikikadiriwa kufika zaidi ya Shilingi Trilioni 5 fursa bado ni kubwa sana. Kwa wastani zaidi ya nusu ya idadi ya watu wazima katika bara la Afrika mpaka sasa wanamiliki simu za mkononi na kwa namna moja au nyingine wana 'access' ya kutumia huduma za ki-benki kupitia simu zao.
Kutokana na usalama na urahisi wa kutumia huduma hizi, biashara nyingi sana zimeruhusu malipo kwa njia ya simu kama namna bora ya kuendesha shughuli zao. Katika maeneo ya mjini ambapo watumiaji wa simu za mkononi ni wengi zaidi, matumizi ya Smartphones yamekua kwa kasi mno.
Time Tickets ni mojawapo ya apps inayolenga kurahisisha huduma za upatikananaji wa habari, taarifa pamoja na kununua tiketi za matukio mbalimbali (events, conferences, exhibitions etc) katika kitufe cha simu yako ndani ya muda mfupi.
![]() |
| Moja ya matamasha maarufu Tanzania yaliyotumia huduma ya Time Tickets. |
App hii inayopatikana katika Google Play Store kwa wale watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android, ina huduma nyingi ambazo hazilengi mtumiaji anayetaka kununua tiketi peke yake, kuna mengi zaidi.
Kupitia Time Tickets unaweza kufanya yafuatayo;
- Kufahamu taarifa kuhusu events mbalimbali ndani ya Tanzania
- Kujisajili na kuweza ununua Tiketi za matamasha mbalimbali. Manunuzi yanaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi. (mobile money services)
- Kuhakiki uhalali wa tiketi zako kupitia mfumo wa QR Codes Scanning kwa kutumia Camera ya simu yako
- Kujua idadi ya mauzo ya mauzo ya tiketi kwa mwaandaaji wa tamasha husika pamoja na idadi ya wahudhuriaji kwenye tamasha lako.
- Unaweza ku-share taarifa za event na marafiki zako hivyo ikawa tool muhimu kwa ajili ya kuimarisha Marketing campaign N.K
Angalia tovuti yao kwa kubonyeza link hii Time Tickets Tanzania
Wapate mtandao Facebook kupitia link hii Time Tickets on Facebook
Chini ni picha za wabunifu wa Time Tickets walipohudhuria maonyesho ya Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam siku ya Jumatano.



