Mtuhumiwa wa mauaji Ufaransa alipiga 'selfie' na kichwa cha marehemu!

Jun 28, 2015

France

Unaweza usielewe lengo hasa la muuaji huyo ambaye mpaka sasa bado anatafutwa kwa udi na uvumba na maafisa usalama kote nchini Ufaransa na mataifa shirika. Mauaji hayo yaliyotokea siku chache zilizopita yanaamsha hisia na hofu kubwa ya matukio ya kigaidi yaliyoanza kufutiwa vichwani mwa Wafaransa. Ni miezi sita iliyopita, tukio la mlipuko liligharimu uhai wa watu 17 na kujeruhi wengine wengi.

Mfanyabiashara Herve Cornara 54, aliyeuliwa ana asili ya Uyahudi na alikua ni meneja wa kiwanda cha gesi karibu na mji wa Lyon mashariki mwa Ufaransa.

Tukio lilivyotokea:
Mtuhumiwa wa mauaji alitambulishwa mpaka sasa kama Salhi alikuwa ni msambazaji mizigo wa mara kwa mara katika kiwanda hicho hiyo alikuwa na vibali vya usalama vya kuingia na kutoka ndani ya kiwanda bila taabu yeyote. Salhi amekuwa mwajiriwa wa kiwanda hicho toka mwezi Machi mwaka huu.

Vyanzo vya habari kutoka Ufaransa vinaripoti, mkanda wa video (CCTV) ulionyesha mtuhumiwa akiingia ndani ya kiwanda na bosi aliyeuliwa ambapo katika moja ya gari za 'delivery' ndipo mauaji yalipofanyiwa. Salhi alimuua mtu aliyekuwa nae ndani ya gari kisha kuutoa mwili wake na kuuweka katikati ya geti ambapo geti lilipojifunga lilitenganisha kichwa na kiwiliwili. 

Mtuhumiwa alijaribu kujiua kwa kutaka kulipua kiwanda chote (kiwanda cha gesi) kwa kubamiza gari katika moja ya mitungi ya gesi ingawa kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kupambana na kuuzima mapema kabla madhara hayajawa makubwa.

Man decapitated in terror attack in France

Taarifa za mwanzo za uchunguzi zinaonyesha picha ya mtuhumiwa aliyojipiga na 'kichwa cha marehemu' ilitumwa kwa mtandao wa WhatsApp kwenda namba ya nchini Canada lakini namba hiyo haijaweza kutambulika mpaka sasa mmiliki wake. 

Nchi ya Canada imetoa tamko la kushirikiana na nchi ya Ufaransa kwenye zoezi la kumsaka mtuhumiwa huyo. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israeli yeye ametoa wito wa raia wa Ufaransa wenye asili ya Uyahudi kurudi nchini Israeli mara moja pale inapobidi.
Mashambulio ya kigaidi nchini Ufaransa yamekuwa yakilenga sana raia wenye asili ya Uyahudi katika miaka ya karibuni.



Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team