AFP
Serikali ya Bangladesh imesema itagharimia upasuaji wa kumtibu mwanamume ambaye anaugua ugonjwa unaofanya mtu kupata dutu zinazofanana na mizizi ya mti mwilini.
Waziri wa afya wa Bangladesh Mohammad Nasim alitangaza hilo baada ya kumtembelea Abul Bajandar, hospitalini Alhamisi.
Bw Bajandar anaugua ugonjwa ambao kisayansi unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi.
Ni ugonjwa wa kinasaba ambao humfanya mtu kuota vidutu kwenye ngozi. Hujulikana sana kama “ugonjwa wa binadamu mti”.
Alianza kuota vidutu miaka 10 iliyopita.
“Awali, nilidhani hazina madhara,” Bw Bajandar ameambia AFP.