R.I.P Banza Stone

Jul 17, 2015



Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone', amefariki dunia.


Banza amefariki dunia alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki huyo nyota wa zamani wa Twanga Pepeta na Tot alikuwa amelazwa hospitalini muda mrefu.

Mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka amethibitisha kifo cha Banza Stone.

“Kweli amefariki leo saa saba, baada ya kutoka tu msikitini ndiyo tumepata taarifa hizo za msiba,” alisema Asha Baraka.

R.I.P Banza 
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team