
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hukumu ya kifungo ya miaka 3 jela na faini ya 5m kwa kila mmoja kwa watuhumiwa wawili waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya Ofisi pamoja na Uhujumu wa Uchumi baada ya kupatikana na hatia huku mtuhumiwa mwingine Grey Mgonja (aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha) akiachiwa huru.
Basil Mramba, aliyepata kuwa Waziri wa Fedha pamoja na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa nishati na Madini wamepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo hicho. Kipindi walichokuwa madarakani waliisababishia serikali hasara ya zaidi ya Tshs Bil 11.7
Habari zaidi itafuata.... Kaa nasi!