Walioteka na kuua Askari kituo cha Stakishari-Ukonga wakamatwa

Jul 22, 2015

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwatia mbarini Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa Majambazi waliovamia Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, huku wengine watatu wakiwa wameuwawa katika shambulio la kutupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18. 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team