Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ yu
mgonjwa tena, safari hii ameibuka na kueleza maradhi ambayo yanamsumbua
akisema: ‘Ugonjwa huu utaniua.”“Kichwa kinaniuma sana hasa wakati wa jua kali, mishipa ya kichwa inaniuma sana halafu nasikia kizunguzungu muda wote, sifahamu ni kwa nini,” alisema mwanamuziki huyo akionekana kuwa na maumivu makali.
Banza alisema hataki kuomba msaada wa kuchangiwa fedha ili
kupata matibabu ila anachoomba ni madaktari ambao wanafahamu tiba ya
ugonjwa huo ili wamsaidie kimatibabu.

Si mara ya kwanza kwa Banza kuumwa kwani mara kadhaa alisharipotiwa kuwa hoi kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua.
“Kwa
sasa nipo tu nyumbani, natazama afya yangu, ukweli nahitaji matibabu ya
nguvu ili kunirejesha kwenye hali yangu ya kawaida,” alisema Banza.
LAKINI JE? Unapoumwa si inashauriwa umwone daktari kwa msaada zaidi?
Na PIA; Sera ya sera ya afya ya nchini inasisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya. Umuhimu huonekana kipindi kama hichi.