Mh. Pinda majibu ya namna hii? KWELI?!

Feb 6, 2015




Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo, mtendaji  mkuu wa Serikali Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitetea ushiriki wa watoto wapatao 500 kwenye sherehe hizo akisema ni sehemu ya mfumo wa wanachama wa CCM.
“Susan, utafikiri tulikuwa pamoja. Nilijua tu swali hili lazima litaulizwa. Ila ‘mtoto wa nyoka ni nyoka’. Chama hiki kina mfumo wake ambao umeshuka mpaka kwenye ngazi ya kitu kinaitwa chipukizi,” alisema akijibu swali la mbunge huyo aliyetaka kujua sababu za CCM kutumia watoto kwenye shughuli zake za siasa wakati ina wanachama wapatao milioni 10 kote nchini.
“Chipukizi hawa ni watoto ambao wamezaliwa kutokana na wazazi wana-CCM, ndiyo maana chama kiliwatumia. Sherehe ilikuwa nzuri na ilipendeza sana. Kwa kuwa hawajafikia umri wa kuingia katika masuala ya siasa, halina madhara lile rafiki yangu, pia bado ni wadogo mno na walikuwa wanafurahia gwaride na kuvaa sare tu.”
Lyimo hakuridhishwa na jibu hilo la Waziri Pinda, akisema hakutakiwa kutoa majibu ya aina hiyo na kwamba katika mkusanyiko huo, kulikuwa na watoto ambao wazazi wao siyo wanachama wa CCM.
“Lengo la watoto hawa ni kusoma na siyo kufanya siasa. Iweje mfanye mambo kwa double standard (ndumilakuwili)?” alihoji na baadaye Pinda alitaka suala hilo lisiendelee kujadiliwa.
“Naheshimu maelezo ya Susan, lakini kiacheni chama kiendelee na utaratibu wake. Mfumo wake ndiyo huo, ndivyo ulivyo na sidhani kama kuna haja ya kuendelea kubishana katika suala hili,” alisema Pinda ambaye ofisi yake inasimamia elimu ya msingi na sekondari.
Najitahidi kuamini kila mwanafunzi alileta kitambulisho cha  uanachama cha mzazi wake kuhakikisha uwiano wa maelezo ya Waziri Mkuu na uhalisia.
KARIBU MWEZI OKTOBA!
 
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team