Karibuni
rafiki yangu Mzungu alikuwa Afrika. Taaluma yake ni
uanahabari. Anaipenda sana Afrika na watu wake. Zamani babu aliishi India
na alipinga sana ukoloni. Ana mke na watoto wawili. Shughuli zake humzungusha kila
sehemu. Analijua bara kuliko hata tuliozaliwa huko. Baada ya
sifa na vicheko, ghafla alisuta mapenzi.
“Ningekuwa mmoja wa babu zenu zamani Bwana Freddy ningenyaka wake ishirini. Kila nilikokwenda sikukosa sahiba. Wanataka niwatumie tikiti za ndege. Waje Ulaya waishi raha mustarehe. Ni vigumu sana kuwahimiza dada hawa kwamba maisha yangu si ya kitajiri. Hata ningekuwa tajiri kwetu Ulaya ndoa za mitala haziruhusiwi. Na mke wangu hatofurahi akisikia nina wake wengine!” Inachekesha alivyosema, lakini ndiyo kichuguu cha mchwa hicho. Kuna kaka mwingine naye karejea Afrika Mashariki alikotalii. Mnigeria. Anawavika sana taji Watanzania. Wakarimu. Si wakorofi kama kwao Lagos, anaremba.
“Ningekuwa mmoja wa babu zenu zamani Bwana Freddy ningenyaka wake ishirini. Kila nilikokwenda sikukosa sahiba. Wanataka niwatumie tikiti za ndege. Waje Ulaya waishi raha mustarehe. Ni vigumu sana kuwahimiza dada hawa kwamba maisha yangu si ya kitajiri. Hata ningekuwa tajiri kwetu Ulaya ndoa za mitala haziruhusiwi. Na mke wangu hatofurahi akisikia nina wake wengine!” Inachekesha alivyosema, lakini ndiyo kichuguu cha mchwa hicho. Kuna kaka mwingine naye karejea Afrika Mashariki alikotalii. Mnigeria. Anawavika sana taji Watanzania. Wakarimu. Si wakorofi kama kwao Lagos, anaremba.
Kweli Wanigeria ni
watu wanaojituma sana. Wengi wamesomea shahada tatu kwa mpigo. Wamezagaa ulimwenguni.
Wajuaji. Na huo usafiri kafiri hawakuuanza jana. Sisi tumegundua kuja Ulaya na
kwingineko takriban miaka hamsini tu. Wanigeria wamesafiri na kuishi ugenini
toka karne ya 18.
Walikuwa miongoni mwa Waafrika waliofanya kazi za uaskari doria na ubaharia, bandari za Uingereza - Liverpool, London na Blackpool, karne ya 19. Leo baadhi ya Wanigeria wana shughuli halali na zisizo halali. Wakati nikiishi Brazil, (miaka 20 iliyopita )Waafrika waliokamatwa na dawa za kulevya walikuwa Wanigeria. Sasa hivi wanawake wa Kitanzania wanaoatilishwa na ukahaba wa kishetani na kitumwa -China na Hongkong- wanahadaiwa na kupigwa na makuadi wa Nigeria.
Walikuwa miongoni mwa Waafrika waliofanya kazi za uaskari doria na ubaharia, bandari za Uingereza - Liverpool, London na Blackpool, karne ya 19. Leo baadhi ya Wanigeria wana shughuli halali na zisizo halali. Wakati nikiishi Brazil, (miaka 20 iliyopita )Waafrika waliokamatwa na dawa za kulevya walikuwa Wanigeria. Sasa hivi wanawake wa Kitanzania wanaoatilishwa na ukahaba wa kishetani na kitumwa -China na Hongkong- wanahadaiwa na kupigwa na makuadi wa Nigeria.
Miaka ya karibuni Wanigeria “wameivumbua” Afrika Mashariki hususan Tanzania. Wamewagundua pia wanawake wa Ethiopia, Uganda na Kenya. Wanawapenda wasivyo wakaidi. Upole huu wa mademu wa Afrika Mashariki unawavutia sana. Wanawake wengi wa Kitanzania wameolewa au kuzaa na wanaume wa Kinigeria. Sidhani kuna ubaya wowote ila kinachogutua ni kule kuachwa wakilea watoto.
| Buses in London by F Macha |
Mbali na sifa
msela wetu alizongwa na moja.
“Nimempata bibi
kwenu Tanzania. Ninampenda sana. Niko tayari kujenga naye maisha. Lakini
nieleze. Nimwamini au nisimwamini?”
Nini shida?
Nikamjuza.
“Ah. Wewe
umeshaishi kwingi. Umeshaishi na wanawake wa kigeni. Unafahamu tofauti za
kitamaduni. Siongei Kiswahili. Siwajui wanawake wenu. Ninakunwa kidogo.
Nilistuliwa namna mwanamke huyu alivyonichangamkia na sijamjua vyema.
Tulikutana na kutoka mara moja mbili, ghafla tayari... anataka arusi!”
Lakini si wanawake
wetu tu. Nilipokuwa Marekani ya kusini niliwashangaa wanawake
walivyonipapatikia. Kuna wakati miye na bendi yangu tulikwenda kupiga muziki
Peru. Muziki wa Reggae. Kwa kuwa bendi ilikuwa ya Wabrazili watupu na
mimi pekee mgeni; wenyeji walidhani kwetu Jamaica au Marekani. Niliposema ni
Afrika, mambo yakageuka pumba.
“Afrika bado
mnakula wadudu? Mnakufa njaa? Bado watu wanalala kwenye nyumba za udongo na
nyasi?”
Hamasa
ghafla ikapungua. Mabibi wakabadilika.
Peru na nchi
nyingine za Marekani ya Kusini zina matatizo ya umaskini na maendeleo kama
Afrika. Wanawake wanapoona wageni hushangilia mbalamwezi na ukombozi. Wanaume hali
kadhalika.
Kila demu wa Kizungu anayetongozwa akija Afrika hulalamika lile lile. Jamaa wanataka urafiki wa haraka. Nahau “I love you” hutamkwa upesi upesi baada ya mkutano mmoja tu. Ah na miye, nilipokuwa kijana sikukosa U- Bulicheka pia. Kuna dada wa Kiingereza alitaka nimpeleke kucheza dansi Kariakoo. Nikampeleka. Sasa kwa vile alikuwa akivuta sigara, na miye nikajifanya navuta sigara. Sigara naiweka mdomoni moshi hauingii. Hadi leo n’nashangazwa jinsi wanawake wa Kizungu walivyo wavutaji sugu wa sigara. Ukitaka cha mvunguni sharti uiname. Alipoomba somo la kupika chakula cha Kitanzania, nikampeleka Mwananyamala. Baada ya mahusiano kuiva kama ule ugali aliojaribu kuusonga Uswahilini nikagundua siri ya sifuri. Mwenzangu alikuwa mtalii. Kaja tu kubadili mandhari. Miye nikajenga ghorofa ishirini na tano kichwani. Najua huyu wangu. Nafikiria ndoa na mbingu. Alivyorudi sikumsikia tena. Miaka ishirini baadaye nilikutana naye kaoana na Mzungu mwenzake.
Kinachotakiwa
kufahamika mosi kabisa, jamani, ni utamaduni.
Sisi tunatafuta
mahusiano na wageni shauri ya shida. Wao wanataka mahusiano ya kweli na undani
zaidi.
Kwa vipi?
Kwanza
kabisa Watanzania hatuna tabia ya kuchanganyikana na watu wa mataifa mengine.
Neno sahihi la Kiingereza ni “networking”...Mmh. Neno muhimu sana
katika ulimwengu wa biashara na mahusiano ya kimataifa leo. Humkuti Mtanzania
kaenda mahali pasipo starehe ya kunywa, kula au manufaa ya aina hiyo. Siyo tu
nyumbani; Ughaibuni, vile vile. Inaweza kuwa shughuli ya maonyesho mathalani ya
picha za camera,kuchora, vinyago au sanamu. Mtanzania atakuuliza niende kuangalia
picha nitapata faida gani? Kumbe hajui huko ndiko atakapokutana na watu wa aina
nyingi na nyingine.
Sasa tunapogongana
ghafla na mgeni, siku hiyo hiyo tukamwambia tunampenda sana; kwamba tuoane au
atuchukue kwao, hatuelewi. Je tutaoanaje na hatufahamiani? Je tuna mambo yapi na mangapi yanayopatana? Hapa ndipo
penye kidari na supu.
Utamaduni ndiyo kiini cha kuwaelewa wanadamu ulimwenguni.
Sisi huzingatia
fedha, uchumi, maendeleo na kutaka kitu kipya kitakachotuondoa gizani.
Mzungu huweka kazi mbele kwanza.
| Nikiwa na dada mzawa wa Afrika Kusini, tamasha la Kahawa, Uingereza, Aprili 2013... |
Biashara, nidhamu,
mahusiano na mapenzi ya kweli, baadaye. Wageni wengine
wanaotoka nchi zinazoendelea kama Afrika Kusini, China, Nigeria, Marekani ya
kusini na kadhalika wanao mseto wa hayo mawili juu. Wapo pia wageni
waongo na fedhuli wanaohadaa watoto, wanawake na vijana. Hawa utawajuaje?
Huzionyesha noti za Dola shauri wanajua utaipapatikia kama samaki aliyeonyeshwa
ndoana. Ndiyo janga lililowafika wanafunzi kadhaa wa vyuoni toka Uganda, Kenya,
Rwanda na Tanzania wakalazimishwa kufanya sinema za ngono mwaka jana.
Ikiwa unatafuta huba la hakika, chunguza kwanza maana ya mahusiano. Jaribu kuelewa watu wa mataifa mbalimbali wakoje. Kama lengo lako ni kupata ahueni ya maisha haraka haraka utadhurika tu. Ukitaka mapenzi ya kweli yakubidi uwe mtambuzi wa “itikadi ya kupeana na kubadilishana.” Mwenzio anataka urafiki; je maana yake nini? Kaja kwako, je utamloga akupende au utajenga urafiki wa dhati kwanza?
Hata ikitokea
mkaoana, mahusiano hayatodumu shauri hamjuani kiundani. Huyu anafikiria Dola;
yule anawaza Papai Bivu.