Ilani mpya kwa wana-blogu nchini

Feb 26, 2015

 Image result for pictures of censorship
Katika kuimarisha zaidi sera ya usalama wa mtandao ikiwemo maadili na matumizi sahihi ya mtandao wa intaneti hasa kwa makundi ya vijana na watoto, Kampuni ya Google imefanya marekebisho katika Sera ya Maudhui ambayo hulinda na kuhakikisha matumizi sahihi ya huduma ya Bloga (Blogger) kulingana na dhima husika. 
Kwa kugusia kidogo,
moja ya dhima kubwa ya blogger ni kuwasiliana, kujieleza na uhuru wa mazungumzo. Ingawa pia Bloga imekua muhimu katika miunganisho mipya kati ya watu, upatikanaji na kiungo kikubwa cha usambazi wa habari.

Marekebisho hayo ya Sera ya Maudhui, yamelenga hasa kusitisha Bloga za umma zenye machapisho yenye kuhusisha picha za uchi, nusu uchi, picha zenye kuleta ashkiki au maudhui yeyote ambayo kwa namna moja au nyingine yanachochea 'ponografia' au kuweka viunga (links) vyenye kuelekeza mitandao mingine yenye maudhui ya namna hiyo.

 Image result for pictures of censorship



Tangu kuwekwa kwa chapiisho hilo la mabadiliko, wana-blogu kadhaa duniani wamelaani hatua hii wakiona ni 'Hatua Dhibiti zisizo na maana' na wengine wakisema ponografia sio kosa kisheria, lakini zaidi ya yote, kama wasemavyo Waswahili 'Cha bure kina gharama'

Hata hivyo blogu zenye maudhui yatakayokua yanakinzana na Sera hiyo mpya zimepewa muda wa kufanya marekebisho ikiwemo;
  •  Kufuta picha za uchi au zenye kuleta ashiki ya namna yeyote LA HASHA kuifuta kabisa Blogu hiyo.
  • Iwapo blogu yako haijihusishi au kua na maudhi yeyote ya pornografia ila si salama kwa matumizi ya watoto, unatakiwa kuweka kibao-tahadhari au ilani kuonyesha blogu husika ina maudhui kwa matumizi ya watu wazima tu (kulingana na sheria halali za nchi husika)
  •  Kuifanya blogu yako kuwa ya matumizi binafsi tu. (unaweza kufanya hivyo kwa kutumia kiunga hiki)
  • Blogu yenye picha za uchi itaruhusiwa tu iwapo itakua ya maudhui ya kufundishia, msingi wa kisanii, kielimu, filamu ionyeshayo hali halisi, au kisayansi au ambapo kuna manufaa mengine makubwa kwa umma kutokana na kutoyachukulia maudhui hatua.
Blogu zote zitakazoanzishwa baada ya tarehe 23 Machi, 2015 (ambayo ni siku ya mwisho ya utekelezaji wa mabadiliko hayo) na kwa namna moja au nyingine kukiuka sera husika hatua za kuifungia kabisa blogu hiyo zinachukuliwa pamoja na kuripotiwa katika vyombo husika vya usalama pale itakapobidi.

Kwa nchi ya Tanzania, ambayo katika kipindi cha karibuni imeshuhudia mlipuko mkubwa wa blogu hasa Google-blogu (ambayo ni bure na rahisi zaidi kutumia), sera hii mpya itakua changamoto kubwa hasa ukizingatia kuwa moja ya vyanzo vikubwa ambavyo vimekua vikitumiwa na wana-blogu kuongeza idadi ya watumiaji (traffic) katika blogu zao imekua ni pamoja na uchapishaji wa picha za uchi. Tutarajie nini?. Kwanza uboreshaji wa maudhui ambao utalenga kuongeza idadi ya watumiaji mtandaoni pasipo kutumia njia za mkato.
Lakini pili, dhima ya hasa ya matumizi ya blogu na matumizi ya intaneti yataongeza hatua katika ukuaji kukidhi kiu na haja ya wakati husika (Information Age). 
Unaweza kusoma zaidi kuhusu marekebisho haya yaliyofanywa kupitia kiunga hiki;

Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team