Wachezaji wa Klabu ya Parma kufua wenyewe

Feb 26, 2015

 
''Ndio habari mpya kwa leo'' Alessandro Lucarelli, team captain wa Klabu ya Parma ya nchini Italia alikaririwa alipokua anaongea na chanzo kimojawapo cha habari nchini humo.
''Kila mchezaji itabidi aende na jezi yake nyumbani kwa ajili ya usafi, hali ngumu ya kifedha imesababisha klabu kushindwa kulipia gharama za usafi'' alisema.
Mechi kati ya Parma na Udinese ya Jumapili iliyopita ilibidi kuahirishwa kutokana na klabu ya Parma kushindwa kulipa hata gharama za wahudumu wa uwanja pamoja na maafisa usalama.

Parma ambayo inashika mkia katika ligi ya Seria A, ikiwa na pointi 10 tu imekumbwa na 'dhahma' hiyo kipindi ambacho ndani ya miezi michache tu kumekua na mabadiliko mara mbili ya umiliki wa timu.

Wachezaji hawajakamilishiwa mishahara yao tangu kuanza kwa msimu huku kukiwa na hofu na kushindwa kumaliza mzunguko wa ligi kutokana na ukosefu wa fedha za kujiendesha.

Giampietro Manenti, rais wa sasa wa klabu hiyo amesema katika mechi ijayo ya ugenini dhidi ya Genoa ana uhakika timu itaweza kuwa na usafiri kwa ajili ya wachezaji.


Lucarelli alisema wachezaji watasafiri kwa magari yao binafsi itakapobidi.
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team