Fursa mpya za biashara Tanzania na Msumbiji

May 21, 2015



Mkataba mpya uliosainiwa kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji, Jaime Basilio Monteiro na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania aliyewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe umefungua fursa mpya kubwa za kiushirikiano kati ya nchi hizi mbili, shukrani nyingi kwa ziara ya Raisi wa Msumbiji Filipe Nyussi.

“Hakutakuwa tena na viza kwa Watanzania wanaokwenda Msumbiji. Awali, walilazimika kulipa Dola za Marekani 900 (zaidi ya Sh1.8 milioni) kwa muda wa siku 30 wakati wao walikuwa wanalipa Sh10,000 kwa siku 90. Baada ya mkataba huu, hakutokuwa tena na malipo hayo,” alisema Membe.
Mkataba huo umeondoa pia malipo ya viza kwa muda huo kwa wafanyabiashara, wanadiplomasia pamoja na wananchi wa kawaida lakini wanafunzi wamepewa kipaumbele cha pekee kwani hawatotakiwa kulipa kwa muda wote wa masomo yao

Rais Nyussi aliwasili nchini jana na atafanya ziara ya siku tatu itakayomfikisha pia Zanzibar ambako atazungumza na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohammed Shein kabla ya kuelekea Dodoma ambako atatembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kabla ya kulihutubia Bunge.
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team