Viongozi wa E.A.C kukutana Dar Es Salaam leo

May 13, 2015

Image result for pierre nku

Kuanza kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki leo hapa jijini Dar Es Salaam kunaambatana na shinikizo kubwa kutoka kwa waandaaji wa maandamano wanaompinga Pierre Nkurunzinza nchini Burundi kupewa tiketi ya kushiriki tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wakitaka iwe ukomo wake katika cheo hicho. Nkurunzinza anatarajiwa kugombea urais kwa awamu ya tatu sasa kupitia tiketi ya chama tawala cha CNDD FDD.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila, Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwanadiplomasia wa Marekani kwa Afrika Linda Thomas-Greenfieldwanatarajiwa pia kuhudhuria mkutano huo ambao utahusisha viongozi wa nchi za Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda pamoja na Burundi.
Watu 20 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha katika ghasia hizo.

 


Image result for pierre nku
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team