Hatma ya waziri aliyesinzia mbele ya Rais wa Korea

May 15, 2015

 
Tangu kuingia madarakani alipomrithi baba yake, Kiongozi Mkuu wa North Korea Kim Jong Un hajawa katika mahusiano mazuri na mataifa ya magharibi achia mbali jirani yake 'hasimu' mkubwa South Korea. Taarifa nyingi za kiintelijensia kutoka mashirika mbalimbali zimekuwa zikitutonya kuhusu 'ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, autocracy leadership na megine mengi.
Siku chache zilizopita kulikuwa na taarifa zilizohusisha mauaji ya Waziri wa Ulinzi wa North Korea kutokana na kosa la kusinzia mbele ya Kim Jong Un ambazo zilitolewa na National Intelligence Service (NIS) la Korea Kusini lakini siku chache baadae mmoja wa wasemaji wa shirika hilo hilo alikanisha tena habari hizo kwa kusema Hyon Yong Chol aliondolewa katika cheo chake lakini hawakuwa na uthibitisho wa kuuliwa kwake.
Mkanganyiko huu wa habari unaonyesha bado ni namna gani usiri mkubwa bado unatawala katika siasa ya nchini Korea Kaskazini achilia mbali uhasama uliopo kati yao na nchi washirika wa mataifa ya magharibi.

hyon yong
Waziri Hyon Yong Chol




Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team