Mafuriko Kenya

May 13, 2015


 A picture showing submerged Kenya Power Nairobi

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayonyesha katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, yamewaua watu kumi na wawili. Polisi imesema ukuta wa msikiti mmoja ulioko katika mtaa wa mabanda wa Fuata Nyayo mjini Nairobi ulianguka na kuwaua watu kumi. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Nairobi Benson Kibue amesema watu wengine wawili walisombwa na mafuriko. Bararaba nyingi za mji huo zimejaa maji kutokana na mafuriko hayo na miundo mbinu mibovu ya mabomba ya kupitishia maji taka yamelaumiwa kwa kuzifanya barabara hizo kutopitika.
Jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania ni mojawapo ya sehemu zilizoathiriwa vibaya pia na mvua ambazo zimekuwa zikiendelea kunyesha mfululizo kwa siku kadhaa sasa na kuharibu miundombinu, makazi na kusababisha hasara kubwa.
Share on :
 
Copyright © 2015 Raizoni Blog
Distributed By My Blogger Themes | Design By SPARTO Inc Team